15 Juni 2025 - 13:16
Source: Parstoday
Pezeshkian: Israel inahujumu juhudi za kuimarisha amani, utulivu na usalama

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja mashambulio ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kuwa ni ushahidi wa dhati ya kijinai ya utawala huo ghasibu na kusema: Tangu niingie madarakani kama Rais, nimekuwa nikijaribu kuimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo hili, lakini utawala wa Kizayuni unavuruga kwa kufanya hujuma katika kila eneo tulilokaribia kukfanikisha jambo fulani.

Rais Masoud Pezeshikian amesema hayo usiku wa kuamkia leo katika mazungumzo ya simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman na kumshukuru kwa kumpigia simu ili kuonesha masikitiko yake kutokana na shambulio la kigaidi la Israel nchini Iran. 

Rais Pezeshkian amesema: "Ninaona ni muhimu, kwanza kabisa, kukushukuru kwa dhati kwa ushirikiano wa kidugu na wa dhati wa Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitakatifu na taasisi nyingine za Saudia kwa kutoa huduma nzuri kwa mahujaji wa mwaka huu. 

Baada ya hapo amezungumzia mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran akisema ni ushahidi wa tabia ya kichokozi ya utawala huo ghasibu na amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa umoja na udugu baina ya nchi za Kiislamu ili kuzuia vitendo vya kihalifu vya utawala wa Kizayuni hususan huko Ghaza.

Amesema: "Kwa kuzingatia nafasi yake katika eneo na ulimwengu wa Kiislamu, Saudi Arabia inaweza kuwa na nafasi madhubuti katika kuimarisha umoja baina ya nchi za Kiislamu kwa ajili ya kutetea haki za Waislamu wote wa eneo hili. Natumai kwamba tunaweza kushirikiana katika kulijaza amani eneo letu hili."

Katika mazungumzo hayo ya simu, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia sanjari na kulaani hujuma za kikatili za utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutoa rambirambi za nchi yake kwa taifa la Iran amesema, Saudia iko pamoja na ndugu zake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na leo hii ulimwengu wote wa Kiislamu unaiunga mkono Iran kwa kauli moja. Amesema: Ninafanya juhudi za kidiplomasia kuishinikiza Israel ikomeshe uhalifu wake.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha